6 BWANA huwategemeza wenye upole,Huwaangusha chini wenye jeuri.
7 Mwimbieni BWANA kwa kushukuru,Mwimbieni Mungu wetu kwa kinubi.
8 Huzifunika mbingu kwa mawingu,Huitengenezea nchi mvua,Na kuyameesha majani milimani.
9 Humpa mnyama chakula chake,Wana-kunguru waliao.
10 Hapendezwi na nguvu za farasi,Wala hairidhii miguu ya mtu.
11 BWANA huwaridhia wao wamchao,Na kuzitarajia fadhili zake.
12 Msifu BWANA, Ee Yerusalemu;Msifu Mungu wako, Ee Sayuni.