3 Msifuni, jua na mwezi;Msifuni, nyota zote zenye mwanga.
4 Msifuni, enyi mbingu za mbingu,Nanyi maji mlioko juu ya mbingu.
5 Na vilisifu jina la BWANA,Kwa maana aliamuru, vikaumbwa.
6 Amevithibitisha hata milele na milele,Ametoa amri wala haitapita.
7 Msifuni BWANA kutoka nchi,Enyi nyangumi na vilindi vyote.
8 Moto na mvua ya mawe, theluji na mvuke,Upepo wa dhoruba ulitendao neno lake.
9 Milima na vilima vyote,Miti yenye matunda na mierezi yote.