7 Msifuni BWANA kutoka nchi,Enyi nyangumi na vilindi vyote.
8 Moto na mvua ya mawe, theluji na mvuke,Upepo wa dhoruba ulitendao neno lake.
9 Milima na vilima vyote,Miti yenye matunda na mierezi yote.
10 Hayawani, na wanyama wafugwao,Vitambaavyo, na ndege wenye mbawa.
11 Wafalme wa dunia, na watu wote,Wakuu, na makadhi wote wa dunia.
12 Vijana waume, na wanawali,Wazee, na watoto;
13 Na walisifu jina la BWANA,Maana jina lake peke yake limetukuka;Adhama yake i juu ya nchi na mbingu.