1 Haleluya.Mwimbieni BWANA wimbo mpya,Sifa zake katika kusanyiko la watauwa.
2 Israeli na amfurahie Yeye aliyemfanya,Wana wa Sayuni na wamshangilie mfalme wao.
3 Na walisifu jina lake kwa kucheza,Kwa matari na kinubi wamwimbie.
4 Kwa kuwa BWANA awaridhia watu wake,Huwapamba wenye upole kwa wokovu.