2 Israeli na amfurahie Yeye aliyemfanya,Wana wa Sayuni na wamshangilie mfalme wao.
3 Na walisifu jina lake kwa kucheza,Kwa matari na kinubi wamwimbie.
4 Kwa kuwa BWANA awaridhia watu wake,Huwapamba wenye upole kwa wokovu.
5 Watauwa na waushangilie utukufu,Waimbe kwa sauti kuu vitandani mwao.
6 Sifa kuu za Mungu na ziwe vinywani mwao,Na upanga mkali kuwili mikononi mwao.
7 Ili kufanya kisasi juu ya mataifa,Na adhabu juu ya kabila za watu.
8 Wawafunge wafalme wao kwa minyororo,Na wakuu wao kwa pingu za chuma.