3 Watakatifu waliopo duniani ndio Walio bora,Hao ndio niliopendezwa nao.
4 Huzuni zao zitaongezekaWambadilio Mungu kwa mwingine;Sitazimimina sadaka zao za damu,Wala kuyataja majina yao midomoni mwangu.
5 BWANA ndiye fungu la posho langu,Na la kikombe changu;Wewe unaishika kura yangu.
6 Kamba zangu zimeniangukia mahali pema,Naam, nimepata urithi mzuri.
7 Nitamhimidi BWANA aliyenipa shauri,Naam, mtima wangu umenifundisha usiku.
8 Nimemweka BWANA mbele yangu daima,Kwa kuwa yuko kuumeni kwangu, sitaondoshwa.
9 Kwa hiyo moyo wangu unafurahi,Nao utukufu wangu unashangilia,Naam, mwili wangu nao utakaa kwa kutumaini.