7 Nitamhimidi BWANA aliyenipa shauri,Naam, mtima wangu umenifundisha usiku.
8 Nimemweka BWANA mbele yangu daima,Kwa kuwa yuko kuumeni kwangu, sitaondoshwa.
9 Kwa hiyo moyo wangu unafurahi,Nao utukufu wangu unashangilia,Naam, mwili wangu nao utakaa kwa kutumaini.
10 Maana hutakuachia kuzimu nafsi yangu,Wala hutamtoa mtakatifu wako aone uharibifu.