1 Ee BWANA, usikie haki, ukisikilize kilio changu,Utege sikio lako kwa maombi yangu,Yasiyotoka katika midomo ya hila.
2 Hukumu yangu na itoke kwako,Macho yako na yatazame mambo ya adili.
3 Umenijaribu moyo wangu, umenijilia usiku,Umenihakikisha usione neno;Nimenuia kinywa changu kisikose,
4 Mintarafu matendo ya wanadamu;Kwa neno la midomo yakoNimejiepusha na njia za wenye jeuri.