3 Umenijaribu moyo wangu, umenijilia usiku,Umenihakikisha usione neno;Nimenuia kinywa changu kisikose,
4 Mintarafu matendo ya wanadamu;Kwa neno la midomo yakoNimejiepusha na njia za wenye jeuri.
5 Nyayo zangu zimeshikamana na njia zako,Hatua zangu hazikuondoshwa.
6 Ee Mungu, nimekuita kwa maana utaitika,Utege sikio lako ulisikie neno langu.
7 Dhihirisha fadhili zako za ajabuWewe uwaokoaye wanaokukimbilia;Kwa mkono wako wa kuumeUwaokoe nao wanaowaondokea.
8 Unilinde kama mboni ya jicho,Unifiche chini ya uvuli wa mbawa zako;
9 Wasinione wasio haki wanaonionea,Adui za roho yangu wanaonizunguka.