5 Nyayo zangu zimeshikamana na njia zako,Hatua zangu hazikuondoshwa.
6 Ee Mungu, nimekuita kwa maana utaitika,Utege sikio lako ulisikie neno langu.
7 Dhihirisha fadhili zako za ajabuWewe uwaokoaye wanaokukimbilia;Kwa mkono wako wa kuumeUwaokoe nao wanaowaondokea.
8 Unilinde kama mboni ya jicho,Unifiche chini ya uvuli wa mbawa zako;
9 Wasinione wasio haki wanaonionea,Adui za roho yangu wanaonizunguka.
10 Wameukaza moyo wako,Kwa vinywa vyao hutoa majivuno.
11 Sasa wametuzunguka hatua zetu,Na kuyakaza macho yao watuangushe chini.