6 Ee Mungu, nimekuita kwa maana utaitika,Utege sikio lako ulisikie neno langu.
7 Dhihirisha fadhili zako za ajabuWewe uwaokoaye wanaokukimbilia;Kwa mkono wako wa kuumeUwaokoe nao wanaowaondokea.
8 Unilinde kama mboni ya jicho,Unifiche chini ya uvuli wa mbawa zako;
9 Wasinione wasio haki wanaonionea,Adui za roho yangu wanaonizunguka.
10 Wameukaza moyo wako,Kwa vinywa vyao hutoa majivuno.
11 Sasa wametuzunguka hatua zetu,Na kuyakaza macho yao watuangushe chini.
12 Kama mfano wa simba atakaye kurarua,Kama mwana-simba aoteaye katika maoteo yake.