35 Nawe umenipa ngao ya wokovu wako,Mkono wako wa kuume umenitegemeza,Na unyenyekevu wako umenikuza.
36 Umezifanyizia nafasi hatua zangu,Na miguu yangu haikuteleza.
37 Nitawafuatia adui zangu na kuwapata,Wala sitarudi nyuma hata wakomeshwe.
38 Nitawapiga-piga wasiweze kusimama,Wataanguka chini ya miguu yangu.
39 Nawe hunifunga mshipi wa nguvu kwa vita,Hunitiishia chini yangu walioniondokea.
40 Naam, adui zangu umewafanya wanipe visogo,Nao walionichukia nimewakatilia mbali.
41 Walipiga yowe, lakini hakuna wa kuokoa,Walimwita BWANA lakini hakuwajibu,