37 Nitawafuatia adui zangu na kuwapata,Wala sitarudi nyuma hata wakomeshwe.
38 Nitawapiga-piga wasiweze kusimama,Wataanguka chini ya miguu yangu.
39 Nawe hunifunga mshipi wa nguvu kwa vita,Hunitiishia chini yangu walioniondokea.
40 Naam, adui zangu umewafanya wanipe visogo,Nao walionichukia nimewakatilia mbali.
41 Walipiga yowe, lakini hakuna wa kuokoa,Walimwita BWANA lakini hakuwajibu,
42 Nikawaponda kama mavumbi mbele ya upepo,Nikawatupa nje kama matope ya njiani.
43 Umeniokoa na mashindano ya watu,Umenifanya niwe kichwa cha mataifa.Watu nisiowajua walinitumikia.