4 Kamba za mauti zilinizunguka,Mafuriko ya uovu yakanitia hofu.
5 Kamba za kuzimu zilinizunguka,Mitego ya mauti ikanikabili.
6 Katika shida yangu nalimwita BWANA,Na kumlalamikia Mungu wangu.Akaisikia sauti yangu hekaluni mwake,Kilio changu kikaingia masikioni mwake.
7 Ndipo nchi iliyotikisika na kutetemeka,Misingi ya milima ikasuka-suka;Ikatikisika kwa sababu alikuwa na ghadhabu.
8 Kukapanda moshi kutoka puani mwake,Moto ukatoka kinywani mwake ukala,Makaa yakawashwa nao.
9 Aliziinamisha mbingu akashuka,Kukawa na giza kuu chini ya miguu yake.
10 Akapanda juu ya kerubi akaruka,Naam, aliruka upesi juu ya mabawa ya upepo.