42 Nikawaponda kama mavumbi mbele ya upepo,Nikawatupa nje kama matope ya njiani.
43 Umeniokoa na mashindano ya watu,Umenifanya niwe kichwa cha mataifa.Watu nisiowajua walinitumikia.
44 Kwa kusikia tu habari zangu,Mara wakanitii.Wageni walinijia wakinyenyekea.
45 Wageni nao walitepetea,Walitoka katika ngome zao wakitetemeka.
46 BWANA ndiye aliye hai;Na ahimidiwe mwamba wangu;Na atukuzwe Mungu wa wokovu wangu;
47 Ndiye Mungu anipatiaye kisasi;Na kuwatiisha watu chini yangu.
48 Huniponya na adui zangu;Naam, waniinua juu yao walioniinukia,Na kuniponya na mtu wa jeuri.