46 BWANA ndiye aliye hai;Na ahimidiwe mwamba wangu;Na atukuzwe Mungu wa wokovu wangu;
47 Ndiye Mungu anipatiaye kisasi;Na kuwatiisha watu chini yangu.
48 Huniponya na adui zangu;Naam, waniinua juu yao walioniinukia,Na kuniponya na mtu wa jeuri.
49 Basi, BWANA, nitakushukuru kati ya mataifa,Nami nitaliimbia jina lako.