1 Mbingu zauhubiri utukufu wa Mungu,Na anga laitangaza kazi ya mikono yake.
2 Mchana husemezana na mchana,Usiku hutolea usiku maarifa.
3 Hakuna lugha wala maneno,Sauti yao haisikilikani.
4 Sauti yao imeenea duniani mwote,Na maneno yao hata miisho ya ulimwengu.Katika hizo ameliwekea jua hema,