1 Mbona mataifa wanafanya ghasia,Na makabila wanatafakari ubatili?
2 Wafalme wa dunia wanajipanga,Na wakuu wanafanya shauri pamoja,Juu ya BWANA,Na juu ya masihi wake,
3 Na tuvipasue vifungo vyao,Na kuzitupia mbali nasi kamba zao.
4 Yeye aketiye mbinguni anacheka,Bwana anawafanyia dhihaka.
5 Ndipo atakaposema nao kwa hasira yake,Na kuwafadhaisha kwa ghadhabu yake.