6 Nami nimemweka mfalme wanguJuu ya Sayuni, mlima wangu mtakatifu.
7 Nitaihubiri amri; BWANA aliniambia,Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa.
8 Uniombe, nami nitakupa mataifa kuwa urithi wako,Na miisho ya dunia kuwa milki yako.
9 Utawaponda kwa fimbo ya chuma,Na kuwavunja kama chombo cha mfinyanzi.
10 Na sasa, enyi wafalme, fanyeni akili,Enyi waamuzi wa dunia, mwadibiwe.
11 Mtumikieni BWANA kwa kicho,Shangilieni kwa kutetemeka.