1 Ee BWANA, mfalme atazifurahia nguvu zako,Na wokovu wako ataufanyia shangwe nyingi sana.
2 Umempa haja ya moyo wake,Wala hukumzuilia matakwa ya midomo yake.
3 Maana umemsogezea baraka za heri,Umemvika taji ya dhahabu safi kichwani pake.
4 Alikuomba uhai, ukampa,Muda mrefu wa siku nyingi, milele na milele.
5 Utukufu wake ni mkuu kwa wokovu wako,Heshima na adhama waweka juu yake.