3 Maana umemsogezea baraka za heri,Umemvika taji ya dhahabu safi kichwani pake.
4 Alikuomba uhai, ukampa,Muda mrefu wa siku nyingi, milele na milele.
5 Utukufu wake ni mkuu kwa wokovu wako,Heshima na adhama waweka juu yake.
6 Maana umemfanya kuwa baraka za milele,Wamfurahisha kwa furaha ya uso wako.
7 Kwa kuwa mfalme humtumaini BWANA,Na kwa fadhili zake Aliye juu hataondoshwa.
8 Mkono wako utawapata adui zako wote,Mkono wako wa kuume utawapata wanaokuchukia.
9 Utawafanya kuwa kama tanuru ya moto,Wakati wa ghadhabu yako.BWANA atawameza kwa ghadhabu yake,Na moto utawala.