4 Baba zetu walikutumaini Wewe,Walitumaini, na Wewe ukawaokoa.
5 Walikulilia Wewe wakaokoka,Walikutumaini wasiaibike.
6 Lakini mimi ni mdudu wala si mtu,Laumu ya wanadamu na mzaha wa watu.
7 Wote wanionao hunicheka sana,Hunifyonya, wakitikisa vichwa vyao;
8 Husema, Umtegemee BWANA; na amponye;Na amwokoe sasa, maana apendezwa naye.
9 Naam, Wewe ndiwe uliyenitoa tumboni,Ulinitumainisha matitini mwa mama yangu.
10 Kwako nalitupwa tangu tumboni,Toka tumboni mwa mamangu ndiwe Mungu wangu.