7 Wote wanionao hunicheka sana,Hunifyonya, wakitikisa vichwa vyao;
8 Husema, Umtegemee BWANA; na amponye;Na amwokoe sasa, maana apendezwa naye.
9 Naam, Wewe ndiwe uliyenitoa tumboni,Ulinitumainisha matitini mwa mama yangu.
10 Kwako nalitupwa tangu tumboni,Toka tumboni mwa mamangu ndiwe Mungu wangu.
11 Usiwe mbali nami maana taabu i karibu,Kwa maana hakuna msaidizi.
12 Mafahali wengi wamenizunguka,Walio hodari wa Bashani wamenisonga;
13 Wananifumbulia vinywa vyao,Kama simba apapuraye na kunguruma.