1 Ee BWANA, nakuinulia nafsi yangu,
2 Ee Mungu wangu,Nimekutumaini Wewe, nisiaibike,Adui zangu wasifurahi kwa kunishinda.
3 Naam, wakungojao hawataaibika hata mmoja;Wataaibika watendao uhaini bila sababu.
4 Ee BWANA, unijulishe njia zako,Unifundishe mapito yako,
5 Uniongoze katika kweli yako,Na kunifundisha.Maana Wewe ndiwe Mungu wa wokovu wangu,Nakungoja Wewe mchana kutwa.