6 Ee BWANA, kumbuka rehema zako na fadhili zako,Maana zimekuwako tokea zamani.
7 Usiyakumbuke makosa ya ujana wangu,Wala maasi yangu.Unikumbuke kwa kadiri ya fadhili zako,Ee BWANA kwa ajili ya wema wako.
8 BWANA yu mwema, mwenye adili,Kwa hiyo atawafundisha wenye dhambi njia.
9 Wenye upole atawaongoza katika hukumu,Wenye upole atawafundisha njia yake.
10 Njia zote za BWANA ni fadhili na kweli,Kwao walishikao agano lake na shuhuda zake.
11 Ee BWANA, kwa ajili ya jina lako,Unisamehe uovu wangu, maana ni mwingi.
12 Ni nani amchaye BWANA?Atamfundisha katika njia anayoichagua.