1 Ee BWANA, unihukumu mimi,Maana nimekwenda kwa ukamilifu wangu,Nami nimemtumaini BWANA bila wasiwasi.
2 Ee BWANA, unijaribu na kunipima;Unisafishe mtima wangu na moyo wangu.
3 Maana fadhili zako zi mbele ya macho yangu,Nami nimekwenda katika kweli yako.
4 Sikuketi pamoja na watu wa ubatili,Wala sitaingia mnamo wanafiki.