4 Sikuketi pamoja na watu wa ubatili,Wala sitaingia mnamo wanafiki.
5 Nimelichukia kusanyiko la watenda mabaya,Wala sitaketi pamoja na watu waovu.
6 Nitanawa mikono yangu kwa kutokuwa na hatia,Na kuizunguka madhabahu yako, Ee BWANA
7 Ili niitangaze sauti ya kushukuru,Na kuzisimulia kazi zako za ajabu.
8 BWANA, nimependa makao ya nyumba yako,Na mahali pa maskani ya utukufu wako.
9 Usiiondoe nafsi yangu pamoja na wakosaji,Wala uhai wangu pamoja na watu wa damu.
10 Mikononi mwao mna madhara,Na mkono wao wa kuume umejaa rushwa.