1 Mpeni BWANA, enyi wana wa Mungu,Mpeni BWANA utukufu na nguvu;
2 Mpeni BWANA utukufu wa jina lake;Mwabuduni BWANA kwa uzuri wa utakatifu.
3 Sauti ya BWANA i juu ya maji;Mungu wa utukufu alipiga radi;BWANA yu juu ya maji mengi.
4 Sauti ya BWANA ina nguvu;Sauti ya BWANA ina adhama;
5 Sauti ya BWANA yaivunja mierezi;Naam, BWANA aivunja-vunja mierezi ya Lebanoni;
6 Airusha-rusha kama ndama wa ng’ombe;Lebanoni na Sirioni kama mwana-nyati.