1 BWANA, watesi wangu wamezidi kuwa wengi,Ni wengi wanaonishambulia,
2 Ni wengi wanaoiambia nafsi yangu,Hana wokovu huyu kwa Mungu.
3 Na Wewe, BWANA, U ngao yangu pande zote,Utukufu wangu na mwinua kichwa changu.
4 Kwa sauti yangu namwita BWANANaye aniitikia toka mlima wake mtakatifu.
5 Nalijilaza nikalala usingizi, nikaamka,Kwa kuwa BWANA ananitegemeza.