1 Nimekukimbilia Wewe, BWANA,Nisiaibike milele.Kwa haki yako uniponye,
2 Unitegee sikio lako, uniokoe hima.Uwe kwangu mwamba wa nguvu,Nyumba yenye maboma ya kuniokoa.
3 Ndiwe genge langu na ngome yangu;Kwa ajili ya jina lako uniongoze, unichunge.
4 Utanitoa katika wavu walionitegea kwa siri,Maana Wewe ndiwe ngome yangu.
5 Mikononi mwako naiweka roho yangu;Umenikomboa, Ee BWANA, Mungu wa kweli.
6 Nawachukia wao washikao yasiyofaa yenye uongo;Bali mimi namtumaini BWANA.