3 Ndiwe genge langu na ngome yangu;Kwa ajili ya jina lako uniongoze, unichunge.
4 Utanitoa katika wavu walionitegea kwa siri,Maana Wewe ndiwe ngome yangu.
5 Mikononi mwako naiweka roho yangu;Umenikomboa, Ee BWANA, Mungu wa kweli.
6 Nawachukia wao washikao yasiyofaa yenye uongo;Bali mimi namtumaini BWANA.
7 Na nishangilie, nizifurahie fadhili zako,Kwa kuwa umeyaona mateso yangu.Umeijua nafsi yangu taabuni,
8 Wala hukunitia mikononi mwa adui;Miguu yangu umeisimamisha panapo nafasi.
9 Ee BWANA, unifadhili, maana ni katika dhiki,Jicho langu limenyauka kwa masumbufu,Naam, mwili wangu na nafsi yangu.