1 Mpigieni BWANA vigelegele, enyi wenye haki,Kusifu kunawapasa wanyofu wa moyo.
2 Mshukuruni BWANA kwa kinubi,Kwa kinanda cha nyuzi kumi mwimbieni sifa.
3 Mwimbieni wimbo mpya,Pigeni kwa ustadi kwa sauti ya shangwe.
4 Kwa kuwa neno la BWANA lina adili,Na kazi yake yote huitenda kwa uaminifu.
5 Huzipenda haki na hukumu,Nchi imejaa fadhili za BWANA.