12 Heri taifa ambalo BWANA ni Mungu wao,Watu aliowachagua kuwa urithi wake.
13 Toka mbinguni BWANA huchungulia,Huwatazama wanadamu wote pia.
14 Toka mahali pake aketipoHuwaangalia wote wakaao duniani.
15 yeye aiumbaye mioyo yao woteHuzifikiri kazi zao zote.
16 Hapana mfalme aokokaye kwa wingi wa uwezo,Wala shujaa haokoki kwa wingi wa nguvu.
17 Farasi hafai kitu kwa wokovu,Wala hamponyi mtu kwa wingi wa nguvu zake.
18 Tazama, jicho la BWANA li kwao wamchao,Wazingojeao fadhili zake.