16 Hapana mfalme aokokaye kwa wingi wa uwezo,Wala shujaa haokoki kwa wingi wa nguvu.
17 Farasi hafai kitu kwa wokovu,Wala hamponyi mtu kwa wingi wa nguvu zake.
18 Tazama, jicho la BWANA li kwao wamchao,Wazingojeao fadhili zake.
19 Yeye huwaponya nafsi zao na mauti,Na kuwahuisha wakati wa njaa.
20 Nafsi zetu zinamngoja BWANA;Yeye ndiye msaada wetu na ngao yetu.
21 Maana mioyo yetu itamfurahia,Kwa kuwa tumelitumainia jina lake takatifu.