18 Tazama, jicho la BWANA li kwao wamchao,Wazingojeao fadhili zake.
19 Yeye huwaponya nafsi zao na mauti,Na kuwahuisha wakati wa njaa.
20 Nafsi zetu zinamngoja BWANA;Yeye ndiye msaada wetu na ngao yetu.
21 Maana mioyo yetu itamfurahia,Kwa kuwa tumelitumainia jina lake takatifu.