4 Kwa kuwa neno la BWANA lina adili,Na kazi yake yote huitenda kwa uaminifu.
5 Huzipenda haki na hukumu,Nchi imejaa fadhili za BWANA.
6 Kwa neno la BWANA mbingu zilifanyika,Na jeshi lake lote kwa pumzi ya kinywa chake.
7 Hukusanya maji ya bahari chungu chungu,Huviweka vilindi katika ghala.
8 Nchi yote na imwogope BWANA,Wote wakaao duniani na wamche.
9 Maana Yeye alisema, ikawa;Na Yeye aliamuru, ikasimama.
10 BWANA huyabatilisha mashauri ya mataifa,Huyatangua makusudi ya watu.