8 Nchi yote na imwogope BWANA,Wote wakaao duniani na wamche.
9 Maana Yeye alisema, ikawa;Na Yeye aliamuru, ikasimama.
10 BWANA huyabatilisha mashauri ya mataifa,Huyatangua makusudi ya watu.
11 Shauri la BWANA lasimama milele,Makusudi ya moyo wake vizazi na vizazi.
12 Heri taifa ambalo BWANA ni Mungu wao,Watu aliowachagua kuwa urithi wake.
13 Toka mbinguni BWANA huchungulia,Huwatazama wanadamu wote pia.
14 Toka mahali pake aketipoHuwaangalia wote wakaao duniani.