1 Nitamhimidi BWANA kila wakati,Sifa zake zi kinywani mwangu daima.
2 Katika BWANA nafsi yangu itajisifu,Wanyenyekevu wasikie wakafurahi.
3 Mtukuzeni BWANA pamoja nami,Na tuliadhimishe jina lake pamoja.
4 Nalimtafuta BWANA akanijibu,Akaniponya na hofu zangu zote.
5 Wakamwelekea macho wakatiwa nuru,Wala nyuso zao hazitaona haya.