5 Wakamwelekea macho wakatiwa nuru,Wala nyuso zao hazitaona haya.
6 Maskini huyu aliita, BWANA akasikia,Akamwokoa na taabu zake zote.
7 Malaika wa BWANA hufanya kituo,Akiwazungukia wamchao na kuwaokoa.
8 Onjeni mwone ya kuwa BWANA yu mwema;Heri mtu yule anayemtumaini.
9 Mcheni BWANA, enyi watakatifu wake,Yaani, wamchao hawahitaji kitu.
10 Wana-simba hutindikiwa, huona njaa;Bali wamtafutao BWANA hawatahitaji kitu cho chote kilicho chema.
11 Njoni, enyi wana, mnisikilize,Nami nitawafundisha kumcha BWANA.