1 Ee BWANA, utete nao wanaoteta nami,Upigane nao wanaopigana nami.
2 Uishike ngao na kigao,Usimame unisaidie.
3 Uutoe na mkuki uwapinge wanaonifuatia,Uiambie nafsi yangu, Mimi ni wokovu wako.
4 Waaibishwe, wafedheheshwe,Wanaoitafuta nafsi yangu.Warudishwe nyuma, wafadhaishwe,Wanaonizulia mabaya.
5 Wawe kama makapi mbele ya upepo,Malaika wa BWANA akiwaangusha chini.