14 Nalijifanya kama kwamba ni rafiki au ndugu yangu,Naliinama nikilia kama aliyefiwa na mamaye.
15 Lakini nikijikwaa hufurahi na kukusanyana,Walinikusanyikia watu ovyo nisiowajua,Wananipapura wala hawakomi.
16 Kama wenye mzaha wakikufuru karamuniWananisagia meno.
17 BWANA, hata lini utatazama?Uiokoe nafsi yangu na maharabu yao,Na mpenzi wangu na wana-simba.
18 Nitakushukuru katika kusanyiko kubwa;Nitakusifu kati ya watu wengi.
19 Walio adui zangu bure wasinisimange,Wanaonichukia bila sababu wasining’ong’e.
20 Maana hawasemi maneno ya amani,Na juu ya watulivu wa nchi huwaza hila.