22 Wewe, BWANA, umeona, usinyamaze;Ee Bwana, usiwe mbali nami.
23 Uamke, uwe macho ili kunipatia hukumuKwa ajili ya madai yangu,Mungu wangu na Bwana wangu.
24 Unihukumu kwa haki yako,Ee BWANA, Mungu wangu,Wala wasinisimangize.
25 Wasiseme moyoni, Haya! Ndivyo tutakavyo;Wasiseme, Tumemmeza.
26 Waaibishwe, wafedheheshwe pamoja,Wanaoifurahia hali yangu mbaya.Wavikwe aibu na fedheha,Wanaojikuza juu yangu.
27 Washangilie na kufurahi,Wapendezwao na haki yangu.Naam, waseme daima, Atukuzwe BWANA,Apendezwaye na amani ya mtumishi wake.