1 Kuasi kwake yule mwovu hunena moyoni mwake,Hakuna hofu ya Mungu mbele ya macho yake.
2 Kwa maana hujipendekeza machoni pakeKuwa upotovu wake hautaonekana na kuchukiwa.
3 Maneno ya kinywa chake ni uovu na hila,Ameacha kuwa na akili na kutenda mema.
4 Huwaza maovu kitandani pake,Hujiweka katika njia mbaya; ubaya hauchukii.
5 Ee BWANA, fadhili zako zafika hata mbinguni,Uaminifu wako hata mawinguni.