3 Maneno ya kinywa chake ni uovu na hila,Ameacha kuwa na akili na kutenda mema.
4 Huwaza maovu kitandani pake,Hujiweka katika njia mbaya; ubaya hauchukii.
5 Ee BWANA, fadhili zako zafika hata mbinguni,Uaminifu wako hata mawinguni.
6 Haki yako ni kama milima ya Mungu,Hukumu zako ni vilindi vikuu,Ee BWANA, unawaokoa wanadamu na wanyama.
7 Ee Mungu, jinsi zilivyo na thamani fadhili zako!Wanadamu huukimbilia uvuli wa mbawa zako.
8 Watashibishwa kwa unono wa nyumba yako,Nawe utawanywesha mto wa furaha zako.
9 Maana kwako Wewe iko chemchemi ya uzima,Katika nuru yako tutaona nuru.