1 Usikasirike kwa sababu ya watenda mabaya,Usiwahusudu wafanyao ubatili.
2 Maana kama majani watakatika mara,Kama miche mibichi watanyauka.
3 Umtumaini BWANA ukatende mema,Ukae katika nchi, upendezwe na uaminifu.
4 Nawe utajifurahisha kwa BWANA,Naye atakupa haja za moyo wako.
5 Umkabidhi BWANA njia yako,Pia umtumaini, naye atafanya.
6 Ataitokeza haki yako kama nuru,Na hukumu yako kama adhuhuri.
7 Ukae kimya mbele za BWANA,Nawe umngojee kwa saburi;Usimkasirikie yeye afanikiwaye katika njia yake,Wala mtu afanyaye hila.