14 Wasio haki wamefuta upanga na kupinda uta,Wamwangushe chini maskini na mhitaji,Na kuwaua wenye mwenendo wa unyofu.
15 Upanga wao utaingia mioyoni mwao wenyewe,Na nyuta zao zitavunjika.
16 Kidogo alicho nacho mwenye haki ni boraKuliko wingi wa mali wa wasio haki wengi.
17 Maana mikono ya wasio haki itavunjika,Bali BWANA huwategemeza wenye haki.
18 BWANA anazijua siku za wakamilifu,Na urithi wao utakuwa wa milele.
19 Hawataaibika wakati wa ubaya,Na siku za njaa watashiba.
20 Bali wasio haki watapotea,Nao wamchukiao BWANA watatoweka,Kama uzuri wa mashamba,Kama moshi watatoweka.