18 BWANA anazijua siku za wakamilifu,Na urithi wao utakuwa wa milele.
19 Hawataaibika wakati wa ubaya,Na siku za njaa watashiba.
20 Bali wasio haki watapotea,Nao wamchukiao BWANA watatoweka,Kama uzuri wa mashamba,Kama moshi watatoweka.
21 Asiye haki hukopa wala halipi,Bali mwenye haki hufadhili, hukirimu.
22 Maana waliobarikiwa na yeye watairithi nchi,Nao waliolaaniwa na yeye wataharibiwa.
23 Hatua za mtu zaimarishwa na BWANA,Naye aipenda njia yake.
24 Ajapojikwaa hataanguka chini,BWANA humshika mkono na kumtegemeza.