21 Asiye haki hukopa wala halipi,Bali mwenye haki hufadhili, hukirimu.
22 Maana waliobarikiwa na yeye watairithi nchi,Nao waliolaaniwa na yeye wataharibiwa.
23 Hatua za mtu zaimarishwa na BWANA,Naye aipenda njia yake.
24 Ajapojikwaa hataanguka chini,BWANA humshika mkono na kumtegemeza.
25 Nalikuwa kijana nami sasa ni mzee,Lakini sijamwona mwenye haki ameachwaWala mzao wake akiomba chakula.
26 Mchana kutwa hufadhili na kukopesha,Na mzao wake hubarikiwa.
27 Jiepue na uovu, utende mema,Na kukaa hata milele.