26 Mchana kutwa hufadhili na kukopesha,Na mzao wake hubarikiwa.
27 Jiepue na uovu, utende mema,Na kukaa hata milele.
28 Kwa kuwa BWANA hupenda haki,Wala hawaachi watauwa wake.Wao hulindwa milele,Bali mzao wa wasio haki ataharibiwa.
29 Wenye haki watairithi nchi,Nao watakaa humo milele.
30 Kinywa chake mwenye haki hunena hekima,Na ulimi wake husema hukumu.
31 Sheria ya Mungu wake imo moyoni mwake.Hatua zake hazitelezi.
32 Mtu asiye haki humvizia mwenye haki,Na kutafuta jinsi ya kumfisha.