33 BWANA hatamwacha mkononi mwake,Wala hatamlaumu atakapohukumiwa.
34 Wewe umngoje BWANA,Uishike njia yake,Naye atakutukuza uirithi nchi,Wasio haki watakapoharibiwa utawaona.
35 Nimemwona mtu asiye haki mkali sana,Akijieneza kama mwerezi wa Lebanoni.
36 Nikapita na kumbe! Hayuko,Nikamtafuta wala hakuonekana.
37 Umwangalie sana mtu mkamilifu,Umtazame mtu mnyofu,Maana mwisho wake mtu huyo ni amani.
38 Wakosaji wataangamizwa pamoja,Wasio haki mwisho wao wataharibiwa.
39 Na wokovu wa wenye haki una BWANA;Yeye ni ngome yao wakati wa taabu.